Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Faini mpya wagombea udiwani, ubunge na urais hizi hapa
Habari za Siasa

Faini mpya wagombea udiwani, ubunge na urais hizi hapa

Sanduku la kura
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imeongeza viwango vya faini kwa wagombea watakaofanya makosa ya kimaadili, katika kampeni na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa NEC, jana Jumatano tarehe 27 Mei 2020 jijini Dar es Salaam alibainisha viwango hivyo wakati akizungumzia mabadiliko katika rasimu ya muongozo wa maadili,  katika kampeni na uchaguzi huo.

Dk. Mahera alisema, faini kwa wagombea udiwani watakaofanya makosa, imeongezeka kutoka Sh. 100,000 hadi isiyozidi 150,000, wakati kwa wagombea ubunge ikiongezeka kutoka Sh. 500, 000 hadi isiyozidi 750,000.

Faini ya wagombea urais ikipanda kutoka Sh. 1,000,000, hadi isiyozidi 1,500,000.

“Viwango vya fedha vya faini kwa  mtu anayefanya makosa vimeongezeka, kama mtu atafanya makosa kwenye ngazi ya udiwani, ilikuwa Sh. 100,000 lakini ilionekana kiwango kidogo,  sasa tumeongeza itakuwa isiozidi Sh. 150,000,” alisema Dk. Mahera

“Kwa wabunge ilikuwa Sh. 500,000 lakini tumeongeza isiozidi Sh. 750,000, na kwenye urais ilikwua Sh. 1,000,000, tumeongeza isiozidi Sh. 1,500,000.”

Dk. Mahera alisema mabadiliko mengine yaliyofanyika katika rasimu hiyo, ni uainishaji wa wadau katika muongozo huo.

“Mabadiliko hayo yamelenga kuhakikisha maadili ni shirikishi na yanakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha yanaleta uwazi katika utekelezaji, mojawapo ya changamoto ndogo iliyojitokeza, ilitakiwa tutaje wadau.  Ambao katika rasimu hii tumewataja, Serikali,  vyama vya siasa na NEC, na mambo mengine,” alisema Dk. Mahera.

Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC, alisema mabadiliko hayo yamefanyika baada ya tume hiyo kupokea maoni kutoka kwa wadau wa uchaguzi, juu ya uboreshaji wa kanuni na miongozo ya itakayotumika kwenye uchaguzi huo.

“Kila mdau amepewa muda wa kutosha kuwaislisha maoni yao na mapendekezo ambayo tume iliyapitia na kuzingatia katika rasimu hiyo,” amesema Jaji Kaijage.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!