April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Faini Mbowe, wenzake: 108 Mil zakusanywa usiku kucha

Noti za Elfu Kumi

Spread the love

ZAIDI ya Tsh. 108,262,000 tayari zimekusanywa ndani ya saa 12, tangu faini ya Freeman Mbowe na wenzake kuwa wazi jana tarehe 10 Machi 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Fedha hizo zimekusanywa kutoka kwa wananchi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuelekea lengo la kuwakomboa viongozi hao leo tarehe 11 Machi 2020.

Taarifa iliyotolewa na Chadema leo imeeleza kuwa, mpaka kufika saa 1:20 asubuhi, kiasi hicho cha fedha tayari kimepatikana ikiwa ni pungufu ya Tsh. 246,738,000.

Nguvu ya umma kazini…hadi alfajiri ya leo Jumatano, Machi 11, 2020, mchango kupitia simu na fedha taslimu, umefikia Tsh. 108,262,000. Tunakaribia kufikia nusu. Tuendelee kuchangia na kuhamasishana kuchangia, kwa simu, benki au kutoa taslimu,” imeeleza taarifa hiyo.

Chadema kimeendelea kuhamasisha wanachama wake kuchanga TSh. 350 milioni kwa ajili ya kuwalipa dhamani viongozi wanane wa chama hicho, waliotiwa hatiani jana tarehe 10 Machi 2020 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Viongozi hao walihukumiwa kulipa kiasi hicho au kwenda jela miezi mitano kwa kila kosa. Walitiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo, fedha hizo hazikupatikana jana na hivyo kupelekwa jela mpaka fedha hizo zitakapolitwa.

error: Content is protected !!