Spread the love

 

NI nani kati ya Sagio Mane na Mo Salah atakayeibuka mbambe dhidi ya mwenzake katika Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2021 kati ya Misri na Senegal. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Michuano hiyo inayofanyikia nchini Cameroon, inahitimishwa kuanzia saa 4:00 usiku wa leo Jumapili, tarehe 6 Februari 2022 katika dimba la Stade Olembe.

Fainali hiyo inatizamwa kwa jicho la kipekee hasa ikizingatiwa, inawakutanisha wachezaji wawili nyota wa kikosi cha kwanza cha Liverpool, inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Mane atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal kutafuta ubingwa huo ambao mwaka 2002 na 2019 waliingia fainali na kuukosa huku Salah yeye atawaongoza mafalao wa Misri kusaka ubingwa huo na wote kwa pamoja katika timu ya taifa wanavalia jezi namba 10.

 

Wakiwa Liverpool, Mane huvalia jezi namba 10 huku Salah akivaa jezi namba 11.

Michuano hiyo imeshuhudia wenyewe, Cameroon wakiibuka washindi wa tatu baada ya kuifunga Burkina Faso kwa penati 5-3. Ni baada ya dakika kumalizika kwa kufungana 3-3.

Burkina Faso walitangulia kwa magoli matatu na Cameroon walianza kurejesha magoli hayo ndani ya dakika 20 kuanzia dakika ya 71 hadi dakika 90 zikawa zote zimerejea.

Dakika 30 za nyongeza, zilimalizika kwa kutokufungana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *