Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Fahamu vigezo na mchakato Kiswahili kutambulika kimataifa
Habari Mchanganyiko

Fahamu vigezo na mchakato Kiswahili kutambulika kimataifa

Profesa wa Kiswahii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Aldin Mutembei
Spread the love

 

TAREHE 7 Julai kila mwaka sasa inatambulika kuwa ni siku ya Kiswahili duniani ambapo leo ndiyo mara ya kwanza siku hiyo kusheherekewa tangu kupewa heshima hiyo na Shirika la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mnamo tarehe 23 Novemba, 2021. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea)

Profesa wa Kiswahii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Aldin Mutembei ameeleza vigezo na mchakato wa Kiswahili kufikia hatua hiyo.

Mutembei ameeleza hayo leo Alhamisi tarehe 7 Julai, 2022, katika maadihimisho ya siku ya Kiswahili duniani yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema miongoni mwa vigezo vilivyoangaliwa ni kama lugha inavuka mipaka ya nchi, kuwa na wingi wa watu na idadi ya wazungumzaji wake.

Amesema kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2017 kiswahili kina wazungumzaji milioni 250.
Ameongeza kigezo kingine kilichoangaliwa ni dhima ya lugha katika kuleta amani, umoja na utangamano.

“Na lugha ya Kiswahili ikapata sifa hiyo kwanza kwa kuanza na Tanzania yenyewe kuwa mfano mzuri na hata kuangalia umoja kati ya Tanganyika na Zanzibar na utangamano wa Afrika Mashariki, ndiyo lugha hiyo ikapa heshima,” amesema Mutembei.

Amesema jambo jingine ilikuwa kuangalia lugha katika elimu “na hapa pia Tanzania ikawa mfano kwamba tunaitumia kama lugha ya kufundishia shule ya msingi.”

Amesema baada ya hapo kukawa na vikao mbalimbali vya ndani na nje, “na hapa ndani tunashukuru ofisi ya UNESCO taifa ambao waliandaa andiko na vikao ili jambo hilo kufanyika vizuri.”

Pia alikishukuru Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo yeye mwenyewe nilipata heshima ya kwenda Paris Ufaransa kwaajili ya kutetea andiko la lugha ya Kiswahili.

“Haikuwa rahisi kwasababu tulipambana na watu huko lakini kwa njia ya diplomasia watu wakakubali katika mkutano ule tarehe 21 Februari 2020.”

Pia ameimshukuru ofisi ya balozi ya Tanzania UNESCO ambayo ilifanya kazi kubwa ya kushawishi umoja wa mabalozi uungue mkono andiko la kuomba lugha ya Kiswahili ukubalike.

“Bahati nzuri umoja huo ukiongozwa na balozi wa Kenya ulikubali kwa kauli moja kwamba tunaunga mkono lugha ya Kiswahili iweze kuwa kama lugha ya kutusemea,” amesema Mutembei.

Amesema taratibu za kuandika na kuomba rasmi ulifanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kusaidia mawasiliano.

“Hatimaye Mkutano Mkuu tarehe 23 Novemba 2021 ukatangaza rasmi lugha ya Kiswahili kwamba inapata hadhi na heshima ya kuwa na siku yake ikiungana na lugha zingine sita kubwa duniani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!