Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Fahamu mambo yaliyopo kwenye mkataba LNG uliosaniwa
Tangulizi

Fahamu mambo yaliyopo kwenye mkataba LNG uliosaniwa

Charles Sangwene
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Timu ya majadiliano ya Serikali ya Tanzania katika mkataba hodhi wa mradi wa kusindika Gesi Asilia (LNG), Charles Sangwene, ameweka wazi kile kilichojadiliwa katika mkataba huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Sangwene ameweka wazi hayo leo Jumamosi tarehe 11, Juni, 2022, wakati wa hafla ya utiliaji saini mkataba huo iliyofanyika Ikulu mkoani Dodoma na kushuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti huyo amesema ili mradi huu utekelezekeke ilionekana ni lazima makubaliano ya kimkataba kati ya Serikali na Kampuni zilizogundua gesi hiyo yafikiwe.

Amesema Mkataba wa nchi Hodhi ambao ndiyo utajenga msingi wa uendelezaji wa mradi wa LNG Tanzania, ni makubaliano ya kimaandishi kati ya nchi ambapo mradi unatekelezwa yaani Tanzania na watekelezaji wa mradi au kampuni kutoka nje ya nchi.

“Lengo la mkataba hodhi ni kuweka mfumo wa kimkataba unaolenga mambo mbalimbali ikiwemo ya kibiashara na kiuchumi, kufafanua wajibu wa Serikali na wa wawekezaji na udhibiti wa mradi husika ili kupata manufaa ya mradi kwa pande zote,” amesema Sangwene.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo pia yanaainisha ruzuku mbalimbali, haki, misamaha, viwango na wajibu ambao Serikali ipo tayari kutoa kwa wawekezaji ili mradi utekelezeke kwa ufanisi na kuleta tija kwa pande zote.

Amesema pia mkataba huo umeanisha matarajio ya Serikali kutokana na mradi kupitia kodi, ushuru au ada, ushirikishaji wananchi na fursa za ajira.

Amesema katika majadiliano hayo ni kuhakikisha kwamba Serikali na wananchi wake wamepata mapato na faida stahiki huku tukihakikisha kuwa mradi unatekelezeka kwa mafanikio.

Ameongeza kwa upande wa timu ya Serikali majadiliano hayo yanafanyika kwa kupata huduma ya ushauri kutoka kwa mshauri elekezi, “ambaye amekuwa na mchango katika kuisaidia timu ya majadiliano kutokana na uzoefu anao nao kutoka na kutekeleza mradi kama hiyo kwenye nchi nyingine.”

Amesema mnamo tarehe 11 Oktoba 2021 timu ya majadiliano ya Serikali iliteuliwa na kuanza majadiliano ya mkataba hodhi yaani HGA na timu za kampuni zilizogundua gesi hiyo.

Ameongeza kuwa majadiliano hayo yalianza rasmi tarehe 8 Novemba 2021 na yalizinduliwa na Waziri wa Nishati Januari Makamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mradi huo.

1 Comment

  • Kwanza anzisheni “regulatory agency” itakayosimamia gesi. Tuache kuanza na mikataba bila kuwa na bodi au asasi ya kudhibiti.
    Pili, tuundeni kampuni ya umma ambayo ndiyo itakayoingia mikataba na wawekezaji na iwe na hisa DSE watanzania wawekeze pia. Tuache utegemezi wa wahisani Hao.
    Serikali kuingia mikataba na wawekezaji ni mfumo wa kikoloni ambapo gavana anawapa hatimiliki ya rasilimali na hawezi kuwashitaki wanapovunja sheria za mazingira, udanganyifu, n.k.
    Wawekezaji wa nje wanatushinda kwa sababu wanatudanganya kesi ziende International Arbitration Court.
    Tuweke vipengele, wakifanya uhalifu wachukuliwe hatua nchini.
    Nasikia kule Marekani rasilimali zinabakia 60% umiliki wa kampuni ya Marekani iliyoundwa na serikali baadaye wazawa wananunua hisa kule NASDQ, S & P, au kwingineko.
    Tujenge dhana na tabia ya kujiamini.
    Madini yote tunayajua. Siyo kweli wamegundua wakati tumewapeleka huko wenyewe watafiti. Hii dhana ya kujinyima haki yetu ya msingi ndiyo inayotuletea umasikini. Kwa sababu tunawamilikisha wao kupindukia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!