December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Exim yatangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’

Spread the love

 

BENKI ya Exim imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya  kampeni  ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayoendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya kampeni hiyo  iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano Msaidizi wa Benki hiyo Bi Mariam Mwapinga alisema jumla ya washindi 6 walipatikana kupitia droo hiyo na kujishindia zawadi ya shillingi million sita fedha taslimu.

“Katika droo ya leo jumla ya washindi sita (6) wamepatikana na wameweza kujishindia zawadi za fedha taslimu kiasi cha sh mil 6. Washindi hawa sita watakabidhiwa zawadi zao katika maeneo yao waliopo na tutaendelea na droo kama hizi kila mwezi na washindi wataendelea kuingia kwenye droo itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.’’

“Wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi hizi kila wakapojiwekea akiba ya kuanzi Tsh. 500,000 na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema Bi Mariam wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa pia na muwakilishi kutoka  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo Bi Mariam alisema inalenga kuleta mabadiliko kwenye mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.

“Lengo si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana, tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’ alitaja.

Alitaja akaunti nyingine kuwa ni pamoja na akaunti ya mzalendo inayoendeshwa bila makato ya kila mwezi, akaunti ya haba na haba, akaunti ya faida ambayo inakuruhusu kuweka akiba na kupata riba pamoja na akaunti ya Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya Watoto pamoja na akaunti ya wajasiriamali inayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti tofauti ya kibiashara.

Kwa upande wake  Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bi Bi Neema Tatock alitoa pongezi kwa washindi wa promosheni hiyo huku akiwahamasisha walengwa kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku akiwahakikishia kuwa Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha zoezi la kupata washindi linafanyika kwa kwa uwazi na kwa kufuata misingi halali ya kubahatisha.

error: Content is protected !!