December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Exim yaendesha droo ya pili ya kampeni ya “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’,

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeendesha droo ya pili ya kampeni yake  “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi Novemba inatoa fursa kwa jumla ya washindi 185 miongoni mwa wateja wa benki hiyo wanaotumia kadi zao za Exim Mastercard kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, Simu janja (Smart Phones) na safari zilizolipiwa gharama zote kwenda mapumziko katika mataifa ya Dubai, Uturuki na Afrika Kusini wao pamoja na wenza wao.

Afisa wa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya Kidigitali wa Benki ya Exim, Gregory Malembeka (wa kwanza kushoto) sambamba na maofisa wengine kutoka Bodi ya taifa michezo ya kubahatisha nchini (GBT) wakizungumza na washindi wa droo ya kampeni “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja wake kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uendeshaji wa droo ya pili ya kampeni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Afisa wa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya Kidigitali wa Benki ya Exim, Gregory Malembeka alisema benki hiyo imeridhishwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wake katika matumizi ya kadi hizo kufuatia kampeni hiyo.

“Kampeni hii imeonyesha mafanikio katika hatua yake ya awali kabisa. Imepokelewa kwa mwamko mkubwa kutoka kwa wateja wetu hatua ambayo tumeitafsiri kwamba ni wazi wateja wetu wananufaika na wanafurahia huduma zetu,’’ alisema Bw Malembeka muda mfupi baada ya kufanyika kwa droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya taifa michezo ya kubahatisha nchini (GBT).

Kwa mujibu wa Malembeka kupitia kampeni hiyo kila muamala wenye thamani ya Tsh 100,000/= na zaidi ukiwa umefanyika kwa mara moja zaidi kupitia card ya MasterCard ya benki hiyo muhusika atastahili kushiriki bahati nasibu ya kumpata mshindi.

“Hii ni droo ya pili ya kila ambapo kila wiki wateja 15 wanaobahatika wamekuwa wakipata nafasi ya kujishindia zawadi ya fedha taslimu  TZS. 100,000/=.’’ Alitaja huku akiongeza: “Aidha, kila mwezi kutakuwa na droo ambapo wateja watapata nafasi ya kujishindia simu janja aina ya iPhone 14 pro mpya kabisa huku sifa ya chini katika droo hii ya mwezi ikiwa ni muhusika kufanya matumizi yenye thamani ya TZS 400,000 na zaidi katika risiti moja au kwa jumla.”

Akizungumzia zawadi kuu kwa washindi  wa kampeni hiyo, Malembeka alisema washindi hao watazawadiwa safari ya mapumziko ya siku tano (5) wao pamoja na wenza wao, safari ambayo itagharamiwa kila kitu na benki ya Exim ikiwemo visa, tiketi ya ndege pamoja na pesa za matumizi.

“Hivyo basi mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya kwenda Dubai yeye na mwenza wake na wakiwa huko watapata fursa ya kutembelea vituo mbalimbali ikiwemo ‘Museum Of The Future’ pamoja na Jangwa la Safari. Mshindi wa pili yeye atakwenda nchini Uturuki  na mwenza wake na wakiwa huko watapata fursa ya kutembelea vivutio kadhaa ikiwemo Msikiti maarufu wa Bluu uliopo kwenye jiji la Istanbul,’’ alisema.

Aidha, aliongeza kuwa mshindi wa tatu atapata fursa ya kutembelea nchi ya Afrika Kusini yeye na mwenza wake ambapo wakiwa huko pia watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo ‘Jozi Towers’ na Mlima wa Meza ambao ni maarufu nchini humo  na Afrika kwa ujumla.

error: Content is protected !!