Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko EWURA yazindua miongozo ya kudhibiti ‘bili’ hewa, upotevu wa maji
Habari Mchanganyiko

EWURA yazindua miongozo ya kudhibiti ‘bili’ hewa, upotevu wa maji

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imezindua miongozo ya utendaji kazi wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira, ikiwemo inayodhibiti upotevu wa maji nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Miongozo hiyo imezinduliwa leo tarehe 23 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, katika kikao kazi cha kutathimini ripoti ya utendaji wa mamlaka hizo, kwa mwaka wa fedha wa 2020/21, iliyozinduliwa jana jijini humo na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kuna neno mmerudia mara nyingi hapa, upotevu wa maji, japo umepungua lakini si kwa kiwango kinachoridhisha, tukitoka hapa tuongeze nguvu ya kupambana na hili tatizo sababu imekuwa wimbo wa siku zote. Tuangalie mamlaka zinazofanya vizuri tujifunze ziwe za nje au za ndani twende tukajifunze,” amesema Mhandisi Sanga.

Aidha, Mhandisi Sanga, amezitaka mamlaka hizo kuzipitia upya mita za maji zinazofungwa, ili kubaini kama sio visababishi vya upotevu wa maji.

“Lakini kuna miongozo tukaitumie, huu muongozo wa mita tukautumie. Hii miongozo tusiifungie makabitini, najua tuko vizuri kuandaa miongozo lakini hstuifanyii kazi,” amesema Mhandisi Sanga.

Miongozo iliyozinduliwa ni Muongozo wa Kuandaa Mikakati ya Kupunguza Upotevu wa Maji kwa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira, Muongozo wa Uchaguzi, Upimaji na Matengenezo ya Dira (mita) za Maji, iliyoandaliwa na Ewura.

Muongozo wa mwisho ni wa Uendeshaji Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira, ulioandaliwa na Wizara ya Maji.

Awali, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa EWURA, Mhandisi Exaudi Fatael Maro amesema mamlaka hiyo imeandaa miongozo hiyo ili kudhibiti changamoto zinazokabili sekta ya maji safi na taka, ikiwemo upotevu wa maji.

“Miongozo hii ina lengo la kudhibiti huduma za maji, hususan kuounguza upotevu wa maji ambao ni tatizo kubwa na kupunguza malalamiko ya wananchi tunaowahudumia ambao wakati mwingine wanapata ankara ‘bili, ambazo sio halisi kulingana na matumizi yao,” amesema Maro.

Katika hatua nyingine, Maro ametaja mafanikio ya mamlaka za maji katika kilindi cha mwaka wa fedha wa jana, ikiwemo ongezeko la ukusanyaji mapato kutoka Sh. 307 bilioni (2019/20) hadi kufikia Sh. 344 bilioni (2020/21).

“Kiwango cha ufanisi wa ukusanyaji mapato kimeongezeka kutoka asilimia 95.1 hadi 95.8,” amesema Maro.

Maro ametaja changamoto zinazokabili mamlaka hizo, ikiwemo kutokukidhi kwa uzalishaji maji kulingana na mahitaji ya maeneo husika ambalo kwa mwaka huo wa fedha.

Pia maji yaliyozalishwa kwenye mamlaka ya miji ya makao makuu ya mikoa ilikuwa asilimia 56.2 ya mahitaji yake, huku za makao makuu ya wilaya na miji midogo, ikikusanywa asilimia 32 ya mahitaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!