Thursday , 29 February 2024
Home Habari Mchanganyiko EWURA yatangaza kushusha bei ya Mafuta
Habari Mchanganyiko

EWURA yatangaza kushusha bei ya Mafuta

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti  wa  Huduma  za  Nishati  na  Maji (EWURA), imetangaza kuwa kuanzia tarehe Mosi Julai, 2017 bei ya mafuta itashuka kwa Sh. 37 kutokana na kushuka  kwa gharama  za usafirishaji  wa  mafuta  katika  soko la dunia, anaandika Yasinta  Francis.

Titus  Kaguo, Meneja  Mawasiliano  na Uhusiano  wa  Ewura amesema  kuwa  bei ya jumla na rejareja  zimepungua  kwa mafuta ya aina zote yani  petroli, dizeli  na mafuta  ya taa.

“Kuanzia Julai mwaka huu, bei za jumla za petroli zinapungua kwa Sh. 37 kwa lita sawa na asilimia 1.92, dizeli shilingi 13.7  kwa lita  sawa na asilimia  0.77  na mafuta ya taa shilingi  18.8 sawa na asilimia 1.10.

“Pamoja  na  ongezeko  la  ushuru   wa  mafuta  ya  petroli  la  shilingi  40  kwa  lita, lakini kuanzia Julai mwaka huu bei za mafuta kwenye soko la ndani  zitapungua kwa kiasi kikubwa,” amesema Kaguo.

Ewura imetangaza kuwa, bei ya mafuta ya petroli kuanzia Julai Mosi, 2017 itakuwa ni Sh. 2,014/- Dizeli Sh. 1,874/- na mafuta ya taa Sh. 1,806/-

“Ewura inawataka wanunuzi wahakikishe wanapata  stakabadhi  ya  malipo  inayoonesha  jina la  kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei  kwa  lita, stakabadhi  hiyo  ya  malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta  endapo kutajitokeza malalamiko,” amesema Kaguo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!