Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko EWURA yaanika mamlaka za maji zisizofanya vizuri, wizara yatoa maagizo
Habari Mchanganyiko

EWURA yaanika mamlaka za maji zisizofanya vizuri, wizara yatoa maagizo

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imetaja Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira, zisizofanya vizuri katika utekelezaji majukumu yake, hasa usambazaji wa maji, ikiwemo Mamlaka za Maji Kateshi, Maswa na Vwawa Mlowo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mamlaka hizo zimetajwa leo tarehe 23 Machi 2022, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa kikao cha siku mbili cha kujadili Ripoti ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira, kwa mwaka wa fedha wa 2020/21, uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, Mamlaka ya Maji Kateshi imeshika nafasi ya 58, kati ya mamlaka za maji za 58 za makao makuu ya wilaya na miji midogo. Mwaka wa 2019/20, mamlaka hiyo ilikuwa nafasi ya 37 katika orodha hiyo.

Kwa upande wa Mamlaka ta Maji Maswa, imeshika nafasi ya mwisho kati ya Mamlaka za Maji za Kitaifa saba, wakati Mamlaka ya Maji Vwawa Mlowo, ikishika nafasi ya 25 kati ya Mamlaka za Maji za Miji ya Makao Makuu ya Mikoa saba 26.

Kufuatia matokeo hayo, Mhandisi Sanga ameziagiza mamlaka hizo kuongeza mikakati ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kasi ya usambazaji maji kwa wateja.

Mhandisi Sanga amezitaka bodi za mamlaka hizo, kuongeza kasi ya utendaji ili kuhakikisha malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020 hadi 2025, ya ufikishaji maji kwa wananchi maeneo ya mijini kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85, yanafikiwa kwa muda uliopangwa.

“Hii si kazi mdogi wakati mwingine tunajisahau, unawexa ukatoa maji kwa asilimia 93 kabla ya 2025 lakini kutokana na ongezeko la watu likafanya uonekane umefikisha kwa asilimia chache na usifikishe asilimia 95 ifikapo 2025. Mahitaji yanaongezeka kila siku na watu wanaongezeka,” amesema Mhandisi Sanga.

Aidha, Mhandisi Sanga, amezipongeza mamlaka hizo kwa kuongeza viwango vya uzalishaji maji na ubora wake, pamoja na kudhibiti upotevu wa maji.

Katika hatua nyingine, EWURA imetaja mamlaka za maji zilizofanya vizuri katika vipengele vinne, ambavyo ni uwasilsihaji bora wa tozo ya udhibiti, udhibiti wa upotevu wa maji, zilizofanya viziri katika kutimiza malengo na cha mwisho ni zilizofanya viziri katika utoaji huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.

Mamlaka zilizofanya vizuri katika uwasilishaji tozo ya udhibiti za EWURA ni pamoja na, Kilindoni, Lushoto, Makambako, Mbinga, Mombo,Igunga, Nzega, Arusha na Iringa.

Kwa upande wa mamlaka zilizofanya vizuri katika kudhibiti upotevu wa maji ni pamoja na, Kishapu na Mamlaka ya Maji ya Moshi.

Mamlaka ya Maji ya Wanging’ombe, imetangazwa kufanya vizuri katika kipengele cha utimizaji malengo wa Mamlaka saba za maji za kitaifa.

Mamlaka ya Maji Singida, imetajwa kushika nafasi ya kwanza kati ya mamlaka 26 za maji za miji mikuu ya makao makuu ya mikoa, katika kutimiza malengi yake. Huku Mamlaka ya Maji Makambako, ikishika nafasi ya kwanza kwa kipengele cha kufanya vizuri kwenye utoaji huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!