August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Everton yawabana nyota wake watatu

Leigthton Baines

Spread the love

KLABU ya Everton inayoshiliki Ligi Kuu ya England imefanikiwa kuwaongeza mikataba nyota wake watatu Gareth Barry, Leigthton Baines na kinda anayechipukia katika timu hiyo Mason Holgate kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo baada ya mikataba yao kuelekea ukingoni.

Barry ambaye ni kiungo wa klabu hiyo ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wakati huo huo beki wa pembeni Baines yeye ameongeza mkataba utakaomfanya aweze kukipiga kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2019, wachezaji hao wawili ndio tegemeo kwenye kikosi cha kocha Ronald Koeman kwa sasa.

Naye Holgate baada ya kuwa na kiwango kizuri katika mechi alizocheza kwa msimu, amefanikiwa kusaini mkataba utakaomuwezesha kubaki Goodison Park kwa miaka mitano ijayo huku Koeman akiwa na matarajio makubwa juu ya kinda huyo.

Mikataba hiyo huenda ikawa chachu kwa wachezaji wa kikosi hicho kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya mahasimu wao Liverpool siku ya Jumatatu kwenye Uwanja la Goodison Park huku wakiwa na rekodi ya kupata ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Arsenal.

Everton ambayo kwa sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia alama 23 imekuwa ni timu ambayo inaleta ushindani mkubwa kwenye ligi na kupata matokeo chanya hasa inapokutana na klabu kubwa katika misimu yote iliyoshiliki ligi hiyo.

error: Content is protected !!