Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo ‘Europian Super League’ yaota mbawa baada ya timu sita kujitoa
Michezo

‘Europian Super League’ yaota mbawa baada ya timu sita kujitoa

Spread the love

 

MICHUANO ya Europian Super League haitafanyika tena baada ya klabu sita kutoka nchini England kujitoa kushiriki kutokana na mashabiki na wadau wa soka kupinga michuano hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michuano hiyo ambayo ilikuwa imeanzishwa na timu 12 Barani Ulaya zikiwemo klabu sita kutoka England ambazo ni  Manchester United, Arsenal, Chelsea, Manchester City, Tottenham na Liverpool.

Mwenyekiti wa michuano hiyo, Andrea Agnelli amesema kuwa kujiondoa kwa timu hizo sita nchini England kwenye michuano hiyo kumefanya kushindwa kuendelea kama ilivyopangwa kutokana na shinikizo kubwa waliopata kutoka kwa mashabiki zao.

“Najaribu kubaki kushawishika na ubora wa huu mradi, Lakini nakubali na maanisha, sifikiri kama huu mradi (Europe Super League) utaendelea,” alisema kiongozi huyo.

Baada ya kutangazwa kutaka kuanzishwa kwa michuano hiyo mipya barani Ulaya ambayo ilipangwa kuchezwa katikati ya wiki mashabiki na wadau wengi wameonekana kutokubaliana na jambo hilo na kusema kuwa michuano hiyo haina afya kwa soka bali wamiliki wa klabu hizo wanaangalia fedha kulino mapenzi na mchezo husika.

Kabla ya michuano hiyo kuanza tayari benki JP Morgan kutoka America ilikuwa tayari kutoa kiasi cha dola za kimarekani bilioni 5, sawa na fedha za kitanzania trillion 11.5, huku dhumuni la kuanzisha michuano hiyo ni kuziondoa klabu kwenye ukata wa kifedha mara baada ya janga la Corona.

Ukiachilia timu hizo kutoka England klabu zingine zilizokuwa kwenye mipango na michuano hiyo ni Inter Milani, AC Millan, Juventus, Real Madrid, Barcelona na Atleticol Madrid.

Michuano hiyo ilipanga kushirikisha jumla ya timu 20, huku wadau wengi wa soka waliona kuwa ni kama njama za kutaka kuififisha michuano mikongwe ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!