Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo ‘Europian Super League’ yaondoka na Ed Woodward Man United
Michezo

‘Europian Super League’ yaondoka na Ed Woodward Man United

Ed Woodward
Spread the love

 

MTENDAJI Mkuu wa Manchester United, Ed Woodward ataachana na timu hiyo mwisho wa mwaka 2021, kufuatia kuhusishwa kwake na kuanzishwa kwa michuano mipya Ulaya ‘Europe Super League’ kwa klabu 12. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Manchester United ilikuwa ni moja kati ya timu sita kutoka nchini England ambazo zilikuwa kwenye mpango wa kushiriki michuano hiyo ambayo imepingwa vikali na Shirikisho la Mpira Miguu Dunia (FIFA) na UEFA.

Mashabiki wengi duniani wameipinga michuano hiyo kwa madai kwa haina afya kwa ustawi wa soka bali wamiliki wa klabu hizo waliangalia fedha zaidi kuliko mapenzi na mchezo wenyewe.

Kuondoka kwa mtendaji huyo kumeonekana ni kuwajibika kufuatia kupigwa vikali kwa michuano hiyo mipya kutokuwa na uwelewa wa kutosha juu ya malengo ya mashindano hayo licha ya kujaa utajiri wa kifedha.

Tayari michuano hiyo ilikuwa imeshapa udhamini wa kifedha kutoka Benki ya JP Morgan ya America ambao walikuwa wapo tayari kutoa kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano, sawa na fedha za kitanzania trilioni 11.5.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Manchester United imeeleza kuwa Ed Woodward ataachana na klabu hiyo aliyohudumu kwa miaka 16 toka mwaka 2005 katika nyazifa tofauti.

Katika taarifa ya kuondoka kwake ndani ya Manchester United, Ed Woodward ameeleza kuwa anajisikia fahari kufanya kazi na klabu kubwa kama hiyo katika kipindi cha miaka 16.

“Najisikia furaha kwa kiasi kikubwa kuhudumu hapa Manchester United na ni heshima kufanya kazi na klabu kubwa kwa miaka 16.

“Nawashukuru mashabiki wa Manchester United kwa sapoti yao katika kipindi kizuri,” alisema Ed Woodward.

Wamiliki wa michuani hiyo walieleza kuwa malengo ya kuanzisha jambo hilo ni kiziondoa timu hizo katika ukata wa kifedha mara baada ya kuibuka kwa janga la corona mapema mwaka jana.

Kuondoka kwa mtendaji huyo ndani ya United huwenda kukawafurahisha baadhi ya wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kuipinga michuano hiyo.

Katika kipindi chake cha uongozi ndani ya klabu hiyo kama mtendaji mkuu, Ed Woodward alishaingia kwenye matatizo na mashabiki kutokana na kukwama kwa usajili mbalimbali za wachezaji.

Mwaka 2018 aliyekuwa Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aliingia kwenye matatizo na bosi huyo kwa kusema kuwa matokeo mabaya waliokuwa wanayapata klabu hiyo hakuwa anapaswa kulaumiwa zaidi ya Ed Woodward.

Wakati wa msimu huo wa mwaka 2018 unaanza, Mourinho aliwaeleza mashabiki wa klabu hiyo kwamba wasitegemee makubwa kwenye msimu huo kutokana na kutopata anachokihitaji kutoka kwa bosi huyo.

Mafanikio makubwa aliyopata Ed Woodward kama mtendaji mkuu ndani ya klabu hiyo ni kushinda taji la Europa, FA pamoja na Kombe la Ligi.

Ed Woodward amaefanikiwa kufanya kazi na makocha wanne tofauti kuanzia na David Moyes, Luis Van Gal, Jose Mourinho pamoja na Ole Gunnar Solskjaer.

Mpaka anaachana na timu hiyo bosi huyo, hakuwahi kushinda taji la Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!