May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Euro yanoga, vigogo waanguka

Spread the love

 

HATUA ya 16 bora ya michuano ya Euro imeanza mwisho wa juma lililopita ambapo mpaka sasa imeshapigwa jumla ya michezo minne, huku vigogo wa soka barani humo, Timu ya taifa ya Uholanzi na Ureno zikitupwa nje kwenye michuano hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michezo miwili ya kwanza kwenye hatua hiyo ulipigwa siku ya Jumamosi, ambapo Denmark iliisukuma nje Wales kwa mabao 4-0, huku Italia ikitinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Austria.

Hatua hiyo pia iliendelea tena siku ya jana kwa kupigwa michezo miwili ambayo ilishuhudia vigogo wakisukumwa nje.

Jamhuri ya Czech iliituoa nje, timu ya Taifa ya Uholazi maa baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0, huku bingwa mtetezi Ureno wakiondoshwa mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, dhidi ya Ubeligiji.

Wachezaji wa Ubelgiji wakishangilia ushindi dhidi ya Ureno

Ureno inatoka kwenye michuano hiyo mara baada ya kuingia kwenye 16 kwa mlango wa nyuma (Best Looser), kwenye kundi F, mbele ya Ufaransa na Ujerumani.

Nahodha wa kikosi hiko Cristiano Ronaldo anaondoka kwenye michuano hiyo, huku akiwa kinara kwenye ufungaji mara baada ya kupachika mabao 5, katika michezo minne aliyocheza kwenye michuano hiyo.

Michuano hiyo pia itaendelea tena hii leo kwenye hatua hiyo ya 16 bora, kwa kupigwa michezo miwili, ambapo Crotia itavaana na Hispania huku mabingwa wa Dunia, timu ya Taifa ya Ufaransa itamenyana na Uswizi.

error: Content is protected !!