Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa EU kuacha kuagiza 90% ya mafuta Urusi
Kimataifa

EU kuacha kuagiza 90% ya mafuta Urusi

Spread the love

 

VIONGOZI wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wamekubaliana kupiga marufuku uingizaji wa hadi theluthi mbili ya mafuta kutoka Urusi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makubaliano hayo yamefikiwa katika siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa Umoja huo unaofanyika jijini Brussels nchini Ubelgiji huku mzozo wa Ukraine na Urusi ukidaiwa kutawala mkutano huo.

Taarifa ya makubaliano hayo imetolewa na viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa mashauriano marefu juu awamu mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi.

Katika awamu ya sasa mafuruku hiyo itahusisha mafuta ya Urusi yanayosafirishwa kwa meli kuingia barani Ulaya ambayo ni sawa na asilimia 90 ya mafuta yote kutoka Moscow.

Hata hivyo, asilimia 10 ya mafuta yanayosafirishwa kwa kutumia bomba la Druzhba kwenda mataifa kadhaa ya katikati na mashariki mwa Ulaya hayatawekewa vikwazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!