February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Eto’o kuzindua uwanja wa soka Tanzania

Spread the love

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o anataraajia kuja nchini Tanzania tarehe 10 Oktoba mwaka huu, kuzindua ujenzi wa kiwanja cha mchezo wa mpira wa miguu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Uwanja huo ambao utakuwa unachezewa mpira wa miguu kwa wachezaji watano (Five a side) utajengwa katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Etoo ambae atakuja chini ya udhamini wa Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia ya Catle Lager ambao wanaendesha kampeni maalumu ya inayofahamika kama (Castle Africa 5s).

Mmoja wa wakilishi kutoka TBL alisema kuwa wameamua kuendeleza mchezo huu hapa Tanzania kwa kujenga kiwanja maeneo ya Oysterbay ambacho kitatambulika kama (Castle Africa Five football pitch).

“Hichi kiwanja kwa kweli kitaweza kusaidia kukuza mpira huu, na sisi tunawaambia watanzania hili jambo zuri sana kwa sababu sasa hivi mpira ni sehemu inayotumika kuingiza mapato” alisema mwakilishi huyo.

Eto’o ambaye ameshawahi kutua katika ardhi ya Tanzania zaidi ya mara mbili akiwa na timu ya taifa ya Cameroon walipokuja kucheza na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika michuano tofauti ya kimataifa ambayo ipo katika kalenda ya Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA.

error: Content is protected !!