November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Etienne aita 27 Stars, Kaseke, Ninja ndani

Spread the love

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania Etienne Ndayilagije ameita kikosi chenye wachezaji 27 kitakacho ingia kambini kwa ajili ya kujiwinda na mchezo dhidi ya Tunisi huku akiwajumuisha kikosini kiungo mshambulia wa Yanga Deus Kaseke na beki wa timu hiyo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao hawakuitwa kwenye kikosi hiko muda mrefu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu.. (endelea).

Mchezo huo ambao utachezwa 13 Novemba 2020 nchini Tunisia ambao utakuwa wa kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa huru Afrika ‘AFCON’ inayitarajia kufanyika nchini Cameroon, Januari 2022.

Kikosi hiko ambacho kitaingia kambini kuanzia 6 novemba 2020 kimetangzwa hii leo huku kikiwa na maingizo mapya matatu ambao ni Deus Kaseke, Ninja na Adam Adam ambye ni mshambuliaji kutoka klabu ya Jkt Tanzania.

Adam Adam itakuwa mara yake ya kwanza kuitwa kuitumikia Taifa Stars mara baada ya kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu huu unaoendelea ambapo mpka sasa ameshapachika jumla ya mabao sita na kushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji nyuma ya Prince Dube wa Azam Fc ambaye amefunga mabao saba.

Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi hiko ni makipa Juma Kaseja (Kmc), Metacha Mnata (Yanga), Aishi Manula (Simba) na David Mapigano (Azam Fc) kwa upande wa mabeki walioitwa ni Shomari Kapombe, Mohammed Hussein na Erasto Nyoni wote kutoka Simba.

Brayson David (Kmc), Bakari Nondo (Yanga), Abdallah Kheri (Azam Fc), huku upande wa viungo waliojumuishwa kikosini ni Jonas Mkude (Simba), Himid Mao (Enppi), Feisal Salum (Yanga), Ally Msengi (Stellenbosch Fc), Salum Abubakar (Azam Fc). Mzamiru Yassin na Said Hamisi wote kutoka Simba.

Washambuliaji walioitwa kwenye kikosi hiko ni Ditram Nchimbi (Yanga), Simon Msumva (Diffa el Jadid), Johhn Bocco (Simba), Iddi Nado (Azam Fc), Farid Mussa (Yanga), Thomas Ulimwengu (Tp Mazembe) na Mbwana Samatta kutoka Fenerbache Fc inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uturuki.

Ikumbukwe kwenye michuano hiyo Stars yupo kundi J, pamoja na mataifa ya Libya na Equatorial Guinea.

error: Content is protected !!