Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Michezo ‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu
Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love

 

UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei 29 katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, umetajwa kuwa unaenda kufanya mapinduzi katika tasnia ya filamu nchini na Afrika kwa ujumla. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea). 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Divisheni ya Utangazaji Azam, Yahya Mohamed alisema filamu hiyo ya kiyasansi imeandaliwa katika viwango vya kimataifa.

“Azam kwa kushirikiana na Power Brush Studios, inatangaza kwa fahari kutolewa kwa filamu ya kwanza ya kisayansi iliyotayarishwa nchini. ‘EONII’. Filamu hii ni muhimu inalenga kuonesha vipaji na uwezo mkubwa ndani ya tasnia ya filamu Tanzania, huku ikivutia watazamaji wa kimataifa kwa silimuli asili na kushirikisha wahusika wa ndani ya nchi,” amesema.

Mohamed amesema ‘EONII’ ambayo uandaaji wake umegharimu zaidi ya dola za Marekani 200,000, inaonesha simulizi ya hadithi na utaalam wa kiufundi katika tasnia ya filamu Tanzania na kutoa jukwaa kwa vipaji vya ndani kustawi huku wakitoa burudani kwa wote kuanzia soko la ndani na nje ya mipaka.

“EONII imebeba hadithi ya kuvutia ya ugunduzi wa kisayansi katikati ya uhitaji wa nishati ya uhakika na ombwe kubwa la kukosekana kwako kunakozua taharuki katika jamii husika, madoido ya kisasa yanayotumika kuzungumzia mkasa huo, itabaki kama alama ya furaha mioyoni mwa Watanzania wapenda filamu,” amesema.

Mohamed amesema wamekuzudia kuzindua rasmi filamu hiyo kuanzia mwezi ujao ambapo itaoneshwa katika kumbi za sinema kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Dodoma na Mwanza, na visiwani Zanzibar.

Amesema filamu hiyo ambayo inatarajiwa kungiza fedha mara mbili ya gharama za kuiandaa, imetengenezwa kwa miaka sita, ikiwa ni mpango wa muda mrefu wa Azam, unaolenga kuongeza umaarufu na matumizi ya filamu za ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Studio za Power Brush iliyoandaa filamu hiyo, Eddie Mzale amesema wamewekeza ubunifu na maarifa yote kuandaa filamu hiyo na kwamba wanajivunia hadi kufikia kuzinduliwa.

“Tunaamini filamu hii sio tu itavutia watazamaji ulimwenguni kote lakini pia itakuwa chachu ya ukuaji wa tasnia ya filamu Tanzania. “EONII ni uthibitisho wa vipaji na uwezo wa ajabu ndani ya tasnia yetu ya ndani, ambapo kwa mara ya kwanza tumetengeneza roboti mwenye uwezo wa kupigana kwa silaha kali za moto,” amesema.

Naye mshiriki mkuu wa filamu hiyo Adam Juma alisema filamu hiyo inaenda kuleta mapinduzi katika tasnia hiyo, hivyo kuwataka Watanzania kujitokeza kuangalia pindi ikianza kuoneshwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Piga pesa kupitia Derby ya London Kaskazini kwa kubadhiri na Meridianbet

Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...

BiasharaMichezo

Wikiendi hii ushindi upo Meridianbet na si kwingine

Spread the love USHINDI huu ni wako mteja wa Meridianbet kama mechi...

BiasharaMichezo

Safari ya Gavi kutoka Academy ya Real Betis mpaka Barca

Spread the love  ANITWA Pablo Martín Páez Gavira ‘Gavi’, sasa ni mchezaji...

BiasharaMichezo

SBL yazindua Serengeti Oktoba Festival

Spread the love  KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia...

error: Content is protected !!