March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Eneo la Catalonia latangaza kujitawala

Spread the love

SERIKALI ya eneo la Catalonia nchini Hispania imetangaza kupata ushindi wa kujitawala baada ya wakazi wake kushiriki kwa wingi katika kura ya maoni iliyofanyika jana Jumapili Oktoba 1, anaandika Catherine Kayombo.

Uongozi wa eneo hilo umethibitisha kwamba kura ya ndiyo kwa uhuru wa kujitawala imeshinda kwa asilimia 90, watu milioni 2.02 wakipiga kura ya ndiyo na 176,000 wakipiga kura ya hapana.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Catalonia, Carles Puigdemont, kiwango cha ushiriki katika kura hiyo ya maoni kilifikia 42.3% hali iliyodhiirisha utayari wa raia wa eneo hilo kuenda kinyume na sheria ya kura ya maoni ya kujitawala iliyopigwa marufuku na serikali ya Uhispania.

Katika hatua ya serikali ya Hispania kuzuia ufanyikaji wa kura hiyo, watu zaidi ya 800 wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wapiga kura. Serikali imedai ufanyikaji wa kura hiyo ni ukiukwaji wa sheria za nchi na Catalonia haijakidhi kujitawala kama jamuhuri.

error: Content is protected !!