May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Elon Musk: Mtu tajiri zaidi duniani

Spread the love

KWA mujibu wa taasisi ya Bloomberg Billionaires Index na Forbes Real Time Billionaires, Elon Musk ambaye ni Mmiliki wa Kampuni ya Tesla na SpaceX, ametangazwa kuwa mtu mwenye utajiri zaidi duniani. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Musk anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 185 baada ya hisa zake za kampuni ya SpaceX kuongezeka jana Alhamisi tarehe 7 Januari 2021.

Nafasi hiyo imekuwa ikishikiliwa na mfanyabiashara Jeff Bezos, mwasisi wa Kampuni ya Amazon tangu mwaka 2017.

Taarifa zaidi zinaeleza, kampuni yake ya Tesla inayozalisha magari ya kutumia umeme, imeongeza faida mara dufu na kwa mara na kwanza imefikia Dola za Marekani bilioni 700 Jumatano wiki hii na kuzipiku kampuni za Ford, Volkswagen, Toyota, GM na Hyundai.

error: Content is protected !!