October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Eliud Kipchoge: Binadamu wa kwanza kukimbia km 42 kwa saa 2

Spread the love

MWANARIADHA wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi ya kuwa binadamu wa kwanza kumalizia mbio za Marathon (kilomita 420 ndani ya masaa mawili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kipchoge ameweka rekodi hiyo leo baada ya kumaliza mbio hizo za kilomita 42 baada ya kutumia dakika 1:59:40 katika mashindano ya mbio za INEOS zilizofanyika Vienna, nchini Austria.

Mwanariadha huyo mbali ya kuweka rekodi hiyo ambayo hyaujawahi kuwekwa na binadamu yoyote duniani, mwaka 2017 aliweka rekodi nyingine ya kumaliza kilomita 42 kwa kutumia saa 2:00:25, katika mashindano yaliyofanyika Monza, nchini Italia.

https://youtu.be/O7UR2Qx8Hzs

Kipchoge amefanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kuwashinda wanaridha wengine 41 kutoka katika mataifa mbalimbali walioshiriki mbio hizo.

error: Content is protected !!