Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Elimu ya mkaa endelevu kutolewa kutunza mazingira
Habari Mchanganyiko

Elimu ya mkaa endelevu kutolewa kutunza mazingira

Mkaa endelevu
Spread the love

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na mazingira, Suleiman Sadiq ameshauri elimu zaidi kutolewa kuhusu Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa nchini (TTCS) maarufu kama mkaa endelevu ili watu wengi wafahamu kwamba mradi huo unasaidia kutunza mazingira na siyo vinginevyo. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Akifungua warsha ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuhusu tathmini ya mradi huo unaondeshwa katika vijiji katika 11 ndani ya Wilaya hiyo, Sadiq ambaye pia ni Mbunge wa wilaya hiyo alisema, watu wengi bado wakisikia suala la ukataji mkaa wanadhani kila mara ni kuharibu misitu wakati mradi wa TTCS umeonesha kwamba unatunza misitu pia.

Alisema, watu wengi wana elimu ndogo zaidi kuhusu mkaa endelevu ambapo elimu ya kutosha ikitolewa itasaidia kuondoa kupigana na kupishana maelezo juu ya utunzaji wa misitu kwa ujumla kwa kutumia uvunaji misitu wa elimu ya mkaa endelevu.  

Aidha alisema, sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2014 inapaswa kutumika ili kusaidia mradi wa mkaa endelevu kuendelea katika vijiji vya Wilaya ya Mvomero mkoani hapa sambamba na kulinda mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Sadiq pia alishauri mradi huo kutokana na manufaa yake kupanua wigo zaidi katika Wilaya mbalimbali za mkoa wa Morogoro ili nao wapate kunufaika na utunzaji wa mazingira huku wakiboresha kipato kwa kutumia mkaa endelevu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Jonas Zeeland alisisitiza mradi wa TTCS kuendelea kutoa elimu mara kwa mara kwa jamii ili izidi kuufahamu mradi huo wenye kuleta tija tofauti na wanavyofikiria.

Awali Meneja Mradi wa mradi wa TTCS Charles Leonard alisema, Mapato katika wilaya hiyo yamekuwa ni kidogo sana ukilinganisha na wilaya zingine za mradi ikiwemo Morogoro vijijini na Kilosa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa miundombinu ya barabara na ukosefu wa masoko ya uhakika.

Hivyo alisema kwa sasa wanaangalia namna ya kusogeza wateja kwenye vijiji vya mradi huo vilivyopo wilayani humo.

Hata hivyo aliwashauri madiwani wa Halmashauri hiyo kuona namna ya kijipanga kimikakati ili kuweza kuongeza mapato kwenda sambamba na wilaya zingine zenye mradi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!