October 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Elimu ya bure sekondari palepale’

Wanafunzi wakishangilia, bila shaka watashangilia kama hivyo watakaposikia kauli hii

Spread the love

SERIKALI imesema itaanza kutekeleza ahadi yake ya kutoa elimu ya sekondari bure katika mwaka wa fedha 2015/16. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (CCM).

Katika swali lake, Shekifu alitaka kujua kama tangazo hilo la serikali la kutoa elimu ya sekondari bure ni la kweli na utekelezaji wake utaanza lini.

Kombani amesema tangazo hilo ni la kweli na utekelezaji wake utaanza katika mwaka wa fedha 2015/16.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kibaha Mjini, Francis Koka (CCM), Kombani amesema uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu ni wa kisheria ambao unawataka wadau mbalimbali ndani ya wilaya kuchangia mfuko na fedha zinazokusanywa na kutumika kuboresha elimu kulingana na vipaumbele vya halmashauri husika.

“Sambamba na uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu, uboreshaji wa mfuko huo unafanyika kwa kutumia asilimia tatu ya mapato ya ndani ya halmashauri
na kupitia.

“Kupitia mifuko hii, imeanzishwa Mamlaka ya Elimu nchini ambapo mwanachama huchangia Sh. 500,000 kwa mwaka na kuweza kuomba fedha za kuboresha elimu katika maeneo ambayo wanayapa kipaumbele,” amesema.

Aliupongeza mji wa Kibaha ambao tayari wana mfuko wa elimu ambao umewezesha kupatikana kwa madawati 500 na ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Miembasa na Mwambisi.

Katika swali lake, Koka alitaka kujua mpango wa serikali wa kuboresha mifuko wa elimu iliyoanzishwa katika halmashauri kwa lengo la kuboresha elimu.

error: Content is protected !!