April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Elimu maalum ya kujikinga na corona itolewe kwa walemavu

Spread the love

SERIKALI imeshauriwa kuona namna bora ya kutoa elimu kwa watu wenye walemavu wa kutosikia (viziwi) jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Jimbo la Nyanda za Juu Kusini, Slvahnus Komba alipokuwa akihubiri katika Ibada ya siku ya pili ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

Askofu Komba ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Sabasaba Jijini Dodoma, alisema kuwa kuna umuhimu wa kuangalia kwa kina jinsi ya kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu juu ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Alisema kuwa watu wenye ulemavu wa kutosikia viziwi wanatakiwa kuhakikisha wanapewa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na changamoto wanayokumbana nayo.

“Ushauri wangu kwa serikali nikiwa Kiongozi wa Kiroho naangalia masuala ya Kiroho na kijamii katika taasisi zote za Umma, Serikali na sehemu muhimu Kama hospitali, vituo vya polisi kwenye mabenki pangekuwepo mkalimani ambaye anaweza kutoa huduma kwa lugha ya alama ili kuweza kuwasaidia watu wa jamii hiyo.

“Wapo watu ambao hawajui hususani hao ndugu zetu viziwi, wanakumbana na changamoto kubwa ya kuelewa mambo mfano kipindi kama hiki cha Corona, licha ya kuwa elimu inatolewa nakini Televisheni nyingi hazina wakalimani wa lugha za halama jambo ambalo ni changamoto kwao,” alisema Askofu Komba.

Akizungumzia watu wenye ulemavu wa viungo hususani wasioweza kusimama alisema kuwa miundombinu ya kuweka vitakatisha mikono kwao iboreshwe kwani kuna wakati ndoo za maji tiririka zinakuwa juu na kumfanya mtu huyo kushindwa kupata huduma.

Akizungumzia kuhusu ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona, Askofu Komba alisema kuwa watumishi wa Mungu wanatakiwa kuendelea kumuomba Mungu wakitambua kuwa ugonjwa wa Corona ni wa muda tu.

Katika hatua nyingine, Askofu Komba amewatahadhalisha waumini wake kuona umuhimu wa kutunza chakula walichonacho badala ya kuingiwa na tamaa ya kukiuza.

“Wakati huu siyo wakati wa kuwa na fedha nyingi kwani siyo muda wote fedha inaweza kukusaidia lakini ni vyema kutunza chakula kwani ukiwa na chakula cha kutosha unaweza kuwa na amani kubwa kuliko kuwa na fedha nyingi lakini hauna cha kununua,” alisema Askofu Komba.

error: Content is protected !!