October 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

EAG yaleta maonesho ya wadau wa makazi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Home Expo, Zeno Ngowi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

KATIKA kuendeleza harakati za kupambana na umaskini nchini, hasa katika sekta ya nyumba na makazi, Kampuni ya Tanzania Home Expo (EAG GROUP), inatarajia kuwa na maonyesho makubwa yatakayokutanisha wananchi na wadau. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

EAG hufanya kazi kwa kushirikiana na makampuni mbalimbali nchini kama daraja la kuweza kuwakutanisha wananchi na wadau mbalimbali wa masuala ya mikopo na ardhi, inayotarajiwa kufanyika Mei 29 hadi 31 mwaka huu, katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumzia maonyesho hayo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa EAG, Zeno Ngowi amesema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuleta kwa pamoja watoa huduma mbalimbali kwenye eneo moja na kuiwezesha jamii kupata taarifa muhimu.

Ngowi amesema lengo lingine ni kutoa elimu kwa wananchi watakaohudhuria maonyesho hayo, pia watapata fursa ya kununua viwanja, kupata wachora ramani, vifaa nya ujenzi na kupata fedha za ujenzi kwa kupatiwa mikopo kwa urahisi.

Amesema, “licha ya kupatiwa fursa hizo, pia tumewaalika Wizara ya Aridhi na Manispaa zote pamoja na wataalamu wa sheria za ujenzi kutoa elimu kwa umma”.

Maonyesho hayo ni ya 5 kufanyika Tanzania, ambapo mwaka huu wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 70 kutoka nchini na Ujerumani, Uturuki, China na Kenya.

error: Content is protected !!