Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DUWASA yajivunia miradi ya UVIKO-19 kufikia asilimia 81
Habari Mchanganyiko

DUWASA yajivunia miradi ya UVIKO-19 kufikia asilimia 81

Spread the love

 

KAIMU Meneja Ufundi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Emmanuel Mwakabole amesema utekelezaji wa Mradi wa UVIKO-19 mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 81. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema kazi inaendelea vizuri na tayari wapo hatua za mwisho za kukamilisha mradi huo ili wananchi waweze kufaidi matunda ya Rais wao Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

“Sisi DUWASA tulipokea Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili Miradi ya UVIKO-19 na mpaka sasa tumefikia asilimia 81 ya kazi zote,” amesema Mhandisi Mwakabole

Amesema kazi zilizofanyika mpaka sasa, ni kazi ya uchimbaji wa visima, mitaro na ulazaji bomba na ujenzi wa tanki zimekamilika kwa Mji wa Bahi na Ntyuka isipokuwa maeneo machache yamebakia, kuingiza bomba kwenye tanki na eneo la kukata lami na katika mji wa Bahi kuna eneo la mawe.

“Kwa sasa ujenzi wa tenki la mji wa Bahi lenye ujazo wa lita 200,000 unaendelea na kwa upande wa Ntyuka ujenzi umekamilika. Katika eneo la Ntyuka ufuatiliaji wa route ya kutoa maji kisima kipya umekamilika na uchimbaji wa mtaro pia umeanza,” amesema Mhandisi Mwakabole

Kwa upande wake, Meneja Msaidizi wa Bahi, Khalifa Ismaily amesema kibanda cha kuwekea pampu kiko tayari na umeme tayari wameshalipia upo katika hatua za mwisho.

Katika fedha za UVIKO-19 Serikali ya Tanzania ilipata mkopo wa shilingi trilioni 1.3 kama mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambapo shilingi Bilioni 139.4 ziligaiwa kwa Wizara ya Maji kwa lengo la kuhakikisha zinatumika kuondoa changamoto ya maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!