August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DUWASA wakata maji Soko la Mavunde, wafanyabiashara walia

Maji ya bomba

Spread the love

 

UONGOZI wa Soko la bonanza katika ya kata ya Chamwino umesema kuna uwezekano wa wafanyabiashara na wateja wa soko hilo kukumbwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kukosekana kwa choo cha uhakika pamoja na maji. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwenyekiti wa Soko hilo maarufu kwa jina la Mavunde, Marwa Mwita ameeleza kuwa soko hilo licha ya kuwa na wafanyabiashara wengi huu ni mwezi wa tatu sasa hakuna huduma ya maji kwani yalikatwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira (DUWASA).

Mwita amesema choo cha soko hilo hakina maji kwa takribani miezi mitatu baada ya kukatwa na DUWASA kutokana na uongozi wa jiji kushindwa kulipwa ankra za maji kwa wakati.

“Pamoja na kwamba choo hakina maji na huduma ni mbaya lakini bado uongozi wa jiji unaendelea kutoza ushuru wa sh.200 kwa wateja wa soko hilo na wafanyabiashara na haielezwi kwanini hawakulipia ankra za maji hadi kufikia hatua ya kukata maji ambayo ni huduma umuhimu.

“Uongozi wa soko la Bonanza tumeandika barua ya kuomba jiji irudishe huduma ya ukusanyaji ushuru wa choo kwa viongozi wa soko na barua hiyo ilipelekwa kwa Mwenyekiti wa kata lakini hakina majibu yoyote ya msingi” amesema Mwita.

Mwita amesema kuwa iwapo huduma ya choo itaelekezwa kwa uongozi wa Soko watakusanya ushuru wa choo na kurejesha maji yaliyokatwa na Mamlaka.

Aidha, Mwita amesema licha ya choo kutokuwa na maji bado ameeleza kuwa matundu ya vyoo hayatoshi kwani soko zima ni sita ambapo wanawake matundu 2 na wanaume matundu manne.

error: Content is protected !!