August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Duterte achimba mkwara mzito

Spread the love

“HUU ni mwanzo na mwisho wa kutegemea askari wa nje, nataka sera za kujitegemea, sihitaji nguvu kutoka taifa lolote” ni kauli ya Rodrigo Duterte, Rais wa Ufilipino akitishia kuvunja makubaliano ya kuimarisha ulinzi (EDCA) na Marekani kusini mwa Ufilipino, anaandika Wolfram Mwalongo.

Aidha, amesema ‘hahitaji kuongozwa kama mbwa aliyeshikwa mnyororo’ na kwamba, anataka kuwa huru hivyo kazi ya ulinzi katika taifa lake itafanywa na askari wa nchi yake.

“Sitaki kuona askari yeyote kutoka taifa lolote ndani ya nchi yangu isipokuwa askari wa Ufilipino…….
Huu ni mwanzo na mwisho wa kutegemea askari wa nje nataka sera za kujitegemea sihitaji nguvu kutoka taifa lolote,” amesema Duterte.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wiki hii katika Uwanja wa Ndege wa Manila (Ufilipino) muda mfupi kabla ya kuanza safari ya ziara nchini Japan.
Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1951 na hubadilishwa kila baada ya miaka 10.

Ambapo mara ya mwisho ulisainiwa tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 2014 kati ya Voltaire Gazmin, Waziri wa Ulinzi wa Ufilipino na Philip Goldberg Balozi wa Marekani nchini humo.

Lengo kuu la makubaliano hayo ilikuwa ni kuimarisha Amani na Ulinzi katika ukanda huo ambapo Marekani iliruhusiwa kujenga ngome za muda na kuimarisha ulinzi pia imekuwa ikiisaidia Ufilipino askari, Meli na Ndege za Kivita.

Marekani kupitia mkataba huo itakuwa mstari wa mbele kuisaidia Ufilipino itakapo kumbwa na majanga ya kimazingira au kibinadamu, ingawa uhusiano huo umeonekana kuteteleka tangu Rais Duterte ashike hatamu yakuongoza taifa hilo.

Hata hivyo, kiongozi huyo amekiri wazi kwamba hana mpango wa kuvunja makubariano yote isipokuwa anataka kufanyke marekebisho kwa baadhi ya vipengele katika mkataba huo.

error: Content is protected !!