October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dulla Mbabe ajiweka kando na masubwi

Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’

Spread the love

 

BONDIA wa Tanzania, Abdallah Pazi maarufu kama ‘Dulla Mbabe’ ametangaza rasmi kujiweka kando na masuala ya masubwi mpaka mwakani hii. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Dulla Mbabe amefikia uamuzi huo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kupoteza pambano lake juzi Jumamosi dhidi ya Mjongo Tshimanga Katompa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Bondia huyo rekodi yake imechafuliwa kwa siku za karibuni katika mapambano aliyopigana baada ya kupoteza yote ambapo pambano la mwisho alitwangwa na Mtanzania mwenzi Twaha Kiduku.

“Mwakani ndio nafikiria kurudi ulingoni, ala kwa sasa wacha nipumzike kwanza nitulize akili nijipange upya… ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni” amesema.

Katika pambano lake dhidi ya Mkongo huyo, Dula Mababe alipoteza kwa pointi za majaji wote watatu.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya mabondia wakubwa hapa nchini kama Hassani Mwakinyo na Twaha Kiduku wamempa salamu za pole bondia mwenzao na kumtia hamasa.

“Asikate tamaa kwani hawezi kuwa bigwa bila kupoteza, lakini mchezo una matokeo matatu kushinda, kupoteza na kutoka sare…. hivyo tupo pamoja naye pia asikate tama,” wamesema.

error: Content is protected !!