August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DSE: Wekezeni ili mfaidike

Spread the love

WATANZANIA wametakiwa kuwa na tabia ya kuwekeza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kukuza mitaji yao, anaandika Regina Mkonde.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mary Kinabo, Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kwamba, hisa za DSE zinatarajiwa kuorodheshwa kwenye soko hapo tarehe 12 Julai, 2016.

“Hisa za DSE zitaorodheshwa kwenye soko tarehe 12 Julai 2016, tunaendelea kuhamasisha wananchi kuwekeza kwenye soko letu ili kukuza mitaji yao kwa kuwa soko letu ni la uhakika,” amesema Kinabo.
Amesema, ukubwa wa mtaji umepanda kwa asilimia 7.76 na kufikia Sh. 23.3 trilioni kutoka Sh. 27.7 trilioni.

“Ukubwa wa mtaji makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kilekile cha trilioni 7.9.
Idadi ya mauzo imepanda kwa asilimia 75 na kufikia Tsh 11.6 bilioni kutoka Sh 6.6 bilioni,” amesema.

Na kuwa, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 68 hadi Sh. 1.7 milioni kutoka Sh. 5.4 milioni ambapo wameshauri wananchi wa kada zote kununua hisa ili kuongeza mtaji kwenye soko.

Amesema, kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni CRDB kwa asilimia 49, TBL asilimia 42, TPCC asilimia 2.95.

 

error: Content is protected !!