Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa DRC yaomba kujiunga Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kimataifa

DRC yaomba kujiunga Jumuiya ya Afrika Mashariki

Felix Tshsekedi, Rais wa DRC
Spread the love

NCHI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imeomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Felix Tshsekedi, Rais wa DRC wakati akikagua Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 14 Juni 2019, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi hapa nchini.

Rais Tshsekedi amesema, nchi yake imeomba kujiunga na EAC ili kuimarisha mahusiano na ushirikiano na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

 “Na kwa wale ambao hawafahamu, nchi yangu tayari imeshaomba kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.Maana naona itakuwa jumuiya muhimu sana duniani,” amesema Tshsekedi.

Kuhusu ziara yake hapa nchini, Rais Tshsekedi amesema lengo lake ni  kuthibitisha mahusiano kati ya Tanzania na DRC, ikiwa pamoja na kuangalia namna nzuri ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo.

“Lengo la ziara hii ni kuja kuthibitisha mahusiano kati ya nchi ya Tanzania na ya Congo, na bila shaka namna nzuri ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wetu mzuri ni kupitia ujenzi  wa miundombinu ambao tumeushuhudia leo,” amesema Rais Tshsekedi.

Rais Tshsekedi amesema, ili Tanzania na DRC zinufaike, kuna ulazima wa kuendeleza miundombinu ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi zote.

Aidha, Rais Tshsekedi amempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji kazi wake, na kuahidi kwamba atachukua yale mazuri anayofanya.

Kwa upande wa serikali, Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi namemhakikishia Rais Tshsekedi kwamba Tanzania inaboresha mazingira mazuri ya biashara ikiwemo kurekebisha viwango vya utozaji kodi, ujenzi wa miundombinu na ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam.

Mhandisi Kamwele amesema, serikali kupitia wizara yake imefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa DRC kuhusu mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini ikiwemo eneo la usafirishaji.

“Wizara yangu kila wakati inakaa vikao na wafanyabaishara wa Kongo. Sasa hivi tuna mradi wa kukarabati bandari  ikiwemo kujenga vizuri magati.

“Hili gati namba 1 kama tumeongeza kina kwenda mita 15, ili ije meli yenye uwezo wa kubeba meli yenye kontena 4,000 hadi 6, 000 tofauti na zamani yalikuwa yanakuja 6,000,” amesema Mhandisi Kamwelwe.

Wakati huo huo, Mhandisi Kamwelwe amemshauri Rais Tshsekedi kuwahimiza wananchi wake kuitumia Bandari ya Dar es Salaam akisema kwamba, ni bandari nafuu kuliko bandari za nchi nyingine.

“Kama nilivyo kwamba, mizigo ya kutoka DRC,  Zambia,  Rwanda na Burundi njia ambayo ni rahisi ni kupitia bandari ya Dar kwenda Ulaya na Asia, kwa sababu ukitoka Dar unakwenda bahari ya Hindi Atlantki  kisha Asia  na Ulaya, bandari zingine itabidi uanze na Atlantiki , Hindi baadae Atlantic kwenda Asia na Ulaya. Kwa wafanyabiashara bandari ambayo ni nafuu ni ya DSM,” amesema Mhandisi Kamwelwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!