Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa DRC mguu sawa ndani ya EAC, wakuu wa nchi waijadili
Kimataifa

DRC mguu sawa ndani ya EAC, wakuu wa nchi waijadili

Spread the love

 

WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo tarehe 22 Disemba, 2021 wamekutana na kujadili ajenda ya kuiruhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wake wa saba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hili ni mojawapo ya matukio yenye maana kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii katika eneo la Maziwa Makuu.

Wakuu wa Jumuiya hiyo leo wamepokea ripoti ya uhakiki wa utayari wa DRC kujiunga na EAC na kuwataka mawaziri wa Jumuiya ya Afrika mashariki kuharakisha mchakato wa majadiliano ya mkataba ili kuiwezesha DRC kuwa mwanachama na kuiwasilisha mapema mwaka 2022 wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

DRC – yenye idadi ya watu takribani milioni 92, litakuwa ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi miongoni mwa nchi wanachama na kutaifanya EAC sasa kuwa jumuiya yenye soko la takribani watu milioni 260.

DRC ni kubwa kieneo na inapakana na takribani nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo – kwa maana ya nchi zote kuondoa Kenya. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini.

Hatua hiyo ya wakuu wa EAC kupitia mkutano wao uliofanyika kwa njia ya mtandao leo, ni shemu ya safari ya takribani miaka 10 – iliyoanza wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila na kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki lililoongozwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Peter Mathuki, kati ya Juni na Julai mwaka huu.

Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameonyesha hamu kubwa ya taifa lake kujiunga na jumuiya hiyo na alitumia sehemu kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa taifa lake mwaka huu kueleza namna taifa lake lilivyokuwa tayari kuwa mwanachama mpya wa EAC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!