
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu
MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, amewafutia shtaka la uhujumu uchumi raia sita wa China, wanaofanya kazi katika Kampuni ya Meli ya Sinota Shipping Company. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 18 Juni 2021 na Wakili wa Serikali, Kija Luzuguna, wakati kesi ya uhujumu uchumi Na. 57/2020, ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Rais hao wa China, waliokuwa wanashtakiwa kwa kesi hiyo mahakamani hapo ni, Chengfa Yang (49), Shu Nan (50), Jin Erhao (35), Gu Jugen (57), Ren Yuangqing (55) na Chen Shinguang (45).
Akizungumza mahakamani hapo, Wakili Luzuguna amedai kuwa, DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, aliifuta kesi hiyo na kuwaacha huru raia hao wa China.
Katika kesi hiyo, Wachina hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu, ambayo ni kusimamia genge la uhalifu uliopelekea kupatikana kwa ndege mmoja aina ya tausi, mwenye thamani ya Sh. 1,150,000. Walilodaiwa kufanya tarehe 11 Agosti 2020.
Shtaka la pili ni kukutwa na nyara ya Serikali, kinyume cha sheria, huku la tatu likiwa ni kukutwa na tausi huyo huku wakijua kummiliki ndege huyo ni kinyume cha sheria.
More Stories
Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT