May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DPP awafungulia kesi ya uhujumu uchumi askari watatu

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, imekusudia kuwafungulia mashtaka ya uhujumu uchumu askari watatu wa Wanyama Pori kwenye Pori tengefu la Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).   

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga jana Ijumaa tarehe 15 Januri 2021, imeeleza mbali na askari, watashitakiwa pamoja na watu wengine zaidi ya watano kwa makosa ya uvamizi wa eneo tengefu la pori hilo na kutishia  kutoweka kwa wanyamapori na kuharibu pori hilo linalochangia asilimia 65 ya maji ya mto Rufiji.

Askari hao watashitakiwa kwa kujihusisha na uhalifu kinyume na sheria ya kuzuia makosa ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya ofisi na kushawishi kupewa rushwa.

Askari hao ni Elisante Ako, Vicent Mkuki na Joshua Magesa.

Watuhumiwa wengine ni; wakulima waliovamia eneo hilo ambao ni Samwel Tango, Jobu Mheni, Pascal Mtwango, Bosco Kindanda, Ernest Ngonyani, John Heguye, Fred Mjoge, Devotha Ngonyanina na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipugasa, Mkasiwa Shabani na Paulo Mwambope.

Taarifa ya DPP inaalelza, ofisi yake imepokea jalada la upelelezi wa shauri hilo wa tangu tarehe 2 Desemba 2020 hadi tarehe 13 Januari 2021, ambapo askari hao hawakuchukua hatua kwa wavamizi hao ikiwa wao ndio waliokuwa doria kwenye eneo hilo.

Askari hao wanadaiwa kutowajibika  pamoja na kutengeneza mazingira ya kupokea rushwa kutoka kwa watu wanaodaiwa kuvamia eneo hilo.

error: Content is protected !!