Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DPP amng’ang’ania Abdul Nondo
Habari MchanganyikoTangulizi

DPP amng’ang’ania Abdul Nondo

Spread the love

MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania, Kanda ya Iringa, kesho Jumatano, tarehe 23 Machi 2022, inatarajia kusikiliza rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, wa kumuacha huru aliyekuwa Mwenyekiti Mtandao wa Wananfunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 22 Machi 2022 na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ambao umetoa wakili wa kumuwakilisha Nondo katika rufaa hiyo.

“Kesho kesi ya Abdul Nondo itasikilizwa katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania, masijala ya Iringa, mbele ya Waheshimiwa majaji wa rufani, Lila, Kitusi, na Mwampashi saa 3:00 asubuhi. DPP alikata rufaa baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama uliompa ushindi Nondo,” imesema taarifa ya THRDC.

Rufaa hiyo namna 30/2020, ilifunguliwa na DPP ikiwa ni takribani mwaka mmoja, tangu Nondo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, kuachwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Nondo alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili, ya kuchapisha taarifa za uongo kwa alitekwa nyara maeneo ya Ubungo, 2018 na kuzisambaza mtandaoni.

Huku shtaka lingie likiwa ni kutoa taarifa za uongo kwa Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mafinga, wilayani Mufindi, Koplo Salim, kuwa alitekwa na watu wasiojuliakana na kupelekwa kiwanda cha Pareto Mafinga, mkoani Iringa.

Katika rufaa hiyo, Nondo atawakilishwa na Mawakili wa THRDC, ambao ni Jebra Kambole, Chance Luoga na Paul Kisabo.

1 Comment

  • Mwandishi,
    Hii haieleweki. Baada ya mahakama ya wilaya si unafungua kesi mahakama ya mkoa au kanda. Mahakama kuu ya rufaa, baadaye.
    Sasa, fanya kazi ya kumuulizaza DDP kwa nini kaifungua Mahakama Kuu ya Rufaa?
    Naomba ubobee sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

error: Content is protected !!