March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DPP amfutia Kubenea kesi ya Shonza

Spread the love
MKURUGENZI wa mashitaka ya jinai nchini (DPP), amemfutia mashitaka yaliyokuwa yanamkabili mahakamani, mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akiwasilisha maombi ya kuondoa shitaka hilo, wakili mwandamizi wa serikali, Beatrice Nsana, ameiambia mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi mkoa wa Dodoma, Joseph Emmanuel Fovo kuwa upande wa “Jamhuri hauna tena dhamira ya kuendelea na shitaka ililolifungua dhidi ya Kubenea.” 

“Mheshimiwa Hakimu, kesi hii imekuja hapa mahakamani kwa ajili ya usikilizaji. Lakini upande wa Jamhuri unawasilisha mbele yako maombi ya kuliondoa shauri hili,” alieleza Beatrice.

Alisema, “tunaomba kufanya hivyo, kupitia kifungu cha 91 cha makosa ya jinai. Tunaliondoa shauri hili kwa hiari na bila kushurutishwa na yeyote.”

Kubenea alifunguliwa kesi ya jinai katika mahakama ya wilaya ya Dodoma kwa mara ya kwanza, tarehe 5 Julai mwaka jana baada ya kudaiwa kumshambulia na kumsababishia maumivu makali, mbunge mwenzake wa Viti Maalum (CCM), Juliana Shonza.

Mbele ya mahakama ya Hakimu mfawadhi wa wilaya, James Karayemaha, ilidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kwenye lango kuu la utawala la Bunge, tarehe 3 Julai 2017.

Mahakama ilielezwa kuwa mbunge huyo machachari wa Ubungo, alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu 240 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hakimu Karayemaha alimpa dhamana mshtakiwa kwa kumtaka kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho na barua kutoka serikali ya mtaa ambaye atasaini bondi ya Sh.1 milioni.

Kabla ya kufutiwa mashitaka, tarehe 18 Julai mwaka huu, hakimu Kalamani aliamuru kuiondoa kesi hiyo mahakamani, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kukamilisha upepelezi na kuomba muda wa nyongeza kama sheria inavyoelekeza.

Hata hivyo, mara baada ya kuachiwa huru, jeshi la polisi mkoani Dodoma lilimkamata tena na kumfungulia mashitaka yaleyale, ambapo mahakama ilimpa dhamana mshitakiwa.

Akisoma uamuzi wa kuondolewa kwa shauri hilo, Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, *** Fofo alisema, mahakama yake haina pingamizi na uamuzi wa serikali wa kuondoa kesi yake.

Akasema, mshitakiwa kwa sasa uko huru kuendelea na shughuli zako kama kawaida. Alisema, upande wa mashitaka unaweza  kufungua upya shauri hilo wakati wowote itakapotaka kufanya hivyo.

Katika shauri hilo, Kubenea alikuwa akitetewa na mawakili watano, Izack Mwaipopo, *** Machimbya, Jeremia Mtobesya, Fred Kalonga na James ole Millya.

Akizungua nje ya mahakama baaada ya kufutiwa mashitaka, Kubenea alisema, anamshukuru Mungu kwa hatua hiyo na kwamba hana mpango wowote wa kufungua madai ya fidia ddhidi ya Shonza.

“Haya yamepita. Badala ya kuhangaika na kesi, ninachaongalia sasa ni jinsi ya kuwahudumia wananchi wa Ubungo. Sisi sote ni wanasiasa. Ninasonga mbele,” alieleza.

Aliwashuru wabunge wote wakiwamo wa chama tawala ambao walikuwa wanafuatilia suala hilo kwa nia njema hadi kufikia hapo lilipofika.

error: Content is protected !!