Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DPP aikabidhi BoT fedha, madini yaliyotaifishwa
Habari za Siasa

DPP aikabidhi BoT fedha, madini yaliyotaifishwa

Biswalo Mganga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)
Spread the love

BISWALO Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) ameikabidhi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) madini ya dhahabu, vito mbalimbali na fedha za kigeni, zilizotaifishwa kutoka kwa wahujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Leo tarehe 29 Juni 2019 Jijini Dar es Salaam, Mganga amemkabidhi Dotto James, Katibu Mkuu wa Hazina madini ya dhahabu yenye uzito wa zaidi ya Kg. 18 yenye thamani ya kiasi cha Dola laki 6.6 na vito vya thamani vyenye uzito wa Kg 2849.45, yenye thamani ya dola laki 3.

Mganga amemkabidhi James madini hayo mbele ya Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria na Dotto Biteko, Waziri wa Madini,

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko ameitaka BoT kuzitunza dhahabu hizo.

“BoT muitunze dhahabu hii, kwa kuwa ni wa kweli waaminifu hatuhitaji zile zama za dhahabu bandia zirudiwe,” ameagiza Biteko.

Balozi Mahiga ametoa wito kwa vyombo vya dola pamoja na mahakama kumaliza changamoto ya utoroshaji madini ili rasilimali hizo zisaidie Watanzania.

“Lakini nataka nipongeze wafanyakazi walioko chini yangu ofisi ya DPP na mahakama, muendelee hivyo. Hii ni asilimia ndogo tu ya uhalifu unaoendelea kuhusiana na utoroshaji wa madini, tuongeze jitihada hali na nguvu katika kulinda rasilimali za nchi yetu,” amesema Balozi Mahiga.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mganga amesema madini hayo yalikamatwa na vyombo vya dola yakiwa njiani kutoroshwa kwenda nje ya nchi.

“Katibu mkuu wizara ya fedha hizi ni Kg 18.354 za dhahabu zenye thamani ya dola laki 6.6 nilizosema, walitunza wakati wanatorosha, naomba katibu mkuu nikukabidhi,” amesema Mganga.

James amesema BoT itahifadhi dhahabu hizo hadi pale serikali itakapotoa maelekezo ya matumizi ya madini hayo.

“Nilichokuwa natekeleza kama katibu mkuu hazina ni jukumu langu kuhakikisha nasimamia mali zote za serikali, hiki kilichokuwa kinafanyika hapa ni mali zilizopatikana kupitia ofisi ya DPP, “ amesema James na kuongeza.

“Mali hizi tulizozipata hapa ikiwemo madini na fedha taslimu ni zilizotaifishwa kupitia Ofisi ya DPP, mali zinapotaifishwa zinarudi mikononi mwa serikali vyovyote iwavyo kama kuna kesi inaendelea na serikali ikashinda mali hizi zinakuwa ni za serikali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!