August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dozi ya Ukimwi kutosubiri muda

Spread the love

KUANZI Oktoba mwaka huu, watu watakaogundulika kuwa na virusi vinavosababisha Ukimwi, watapewa dawa ya kupunguza makali hapo hapo badala ya kusubiri kinga zao za mwili kupungua, anaandika Dany Tibason.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi imeitaka serikali kuongeza fedha katika kupambana na ugonjwa huo baada ya wahisani kupunguza misaada yao.

Costantine Kanyasu, mwenyekiti wa kamati hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho amesema,  wafadhili wengi wamepunguza misaada katika kuwahudumia wagonjwa hao hivyo serikali inatakiwa kuongeza fedha.

Amesema, utafiti unaonesha kuwa, walioambukizwa Virusi vya Ukimwi mpaka sasa ni watu milioni 2,400,000 lakini wanaopata dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ni 700,000 pekee.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, serikali imesema itaongeza idadi ya utoaji wa dawa na kufikia wagonjwa milioni 1,1000,000 ifikapo Oktoba mwaka huu na kwamba, bado watu zaidi wa milioni 1.3 watakosa dawa.

“ Kamati imeomba serikali kuongeza fedha kutokana na wafadhili kujitoa au kupunguza misaada yao katika ugonjwa huu, vinginevyo itoe dawa bure kwa wale wanaohitajika kupata bure na iruhusu watu binafsi kuagiza nje na kuziuza kwa bei nafuu ili kufikia malengo,’’ amesema.

Awali, akizungumzia masuala ya chanjo kwa kamati hiyo Dk.Mpoki Ulusubisya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema, chanjo dhidi ya ugonjwa huo bado inahitajika.

Amesema, utafiti uliofanyika unaonesha kuwa, maambukizi  kwa wanawake ni makubwa kwa asilimia 6.25 ikilinganishwa na wanaume wenye  maambukizi asilimia 3.8.

 

error: Content is protected !!