October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dovutwa ang’olewa UPDP 

Fahmi Dovutwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa UPDP

Spread the love

FAHMI Dovutwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha UPDP, ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Imeelezwa, Dovutwa ameng’olewa kwenye nafasi hiyo kwa madai, alikitoa chama hicho katika kushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019.

Kwa mujibu wa Abdalla Mohammed Khamis, Kaimu Mwenyekiti wa UPDP,  Dovutwa amevuliwa uenyekiti na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Khamis amesema Dovutwa amepewa adhabu hiyo kufuatia hatua yake ya kutangaza UPDP hakitashiriki uchaguzi huo, pasina kupewa ridhaa na uongozi wa chama hicho.

Ameeleza kuwa, kitendo hicho ni kinyume na katiba ya UPDP, pia, kimesababisha chama hicho kukosa wenyeviti wa serikali za mitaa.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika pasina ushiriki wa vyama vya upinzani nane, ikiwemo chama cha UPDP.

Vyama hivyo, vilisusa kushiriki uchaguzi huo kwa madai kuwa, mchakato wake ulikiuka kanuni za uchaguzi huo.

 

 

 

 

error: Content is protected !!