Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Donald Trump atokea tundu ya sindano
Habari MchanganyikoKimataifa

Donald Trump atokea tundu ya sindano

Spread the love

 

ALIYEKUWA rais wa Marekani, Donald Trump, ameponea chupuchupu kitiwa hatiani, kutokana na madai ya kuchochea vurugu katika jengo la Bunge, tarehe 6 Januari mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa zinasema, Trump amenusurika kutiwa hatiani baada ya Bunge la Seneti kushindwa kupata theluthi mbili ya kura zilizohitajika, kumuadhibu kiongozi huyo.

Maseneta 57 walipiga kura kumtia hatiani Trump wakiwamo saba kutoka chama chake cha Republican, huku 43 walipiga kura kupinga hatua hiyo. Zilihitajika kura 10 kumtia hatiani.

Baada ya kushindwa kumtia hatiani, Trump alilaani kesi hiyo akiita, ililenga “kumtafuta mabaya.” Hii ilikuwa kesi ya pili dhidi ya Trump.

Kama angetiwa hatiani, Bunge la seneti lingepiga kura dhidi ya kumzuia Trump  kuwania tena nafasi ya rais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Baada ya zoezi la kura kumalizika, Seneta mwandamizi wa chama Republican ndani ya Congress, Mitch McConnel alisema, Trump amekuwa ”akiwajibika” kutokana na kile kilichotokea Capitol.

Awali, alipiga kura dhidi ya kutiwa hatiani kwa Trump akisema, hatua hiyo ni kunyume cha katiba kwa kuwa Trump si rais tena.

McConnell amekuwa akipinga vikali kesi dhidi ya Trump mpaka alipoondoka madarakani tarehe 20 Januari.

Hata hivyo, McConnell alimtahadharisha Trump kuwa bado anaweza kuwajibishwa mahakamani.

Alisema, “si kwamba amekwepa chochote. Tuna mfumo wa kushughulikia jinai katika nchi hii, tuna mashtaka ya raia na marais wa zamani hawana kinga ya kutowajibishwa.”

Rais Joe Biden alisema: ”Wakati kura ya mwisho haikuwezesha Trump kutiwa hatiani, kiini cha mashtaka hakina ubishi.

”Hatua hii ya kusikitisha katika historia yetu imetukumbusha kuwa demokrasia iko hatarini. Na kuwa wakati wote lazima ilindwe.

“Ni lazima kuwa macho na vurugu na kwamba msimamo mkali havina nafasi nchini Marekani. Kila mmoja wetu ana kazi na wajibu kama Wamareani na hasa kama viongozi, kutetea ukweli na kuushinda uongo.”

Katika kuhitimisha, Bunge la wawakilishi wa Democratic walisema itakuwa ni hatari kumuachia Trump.

”Hatari inaweza kuwa kubwa kwa kuwa ukweli mchungu ni kwamba kile kilichotokea tarehe 6 Januari, kinaweza kutokea tena mwakilishi Joe Neguse alisema.

Hata hivyo, wakili wa Trump, Michael van der Veen, ameita kesi hiyo ”maonesho” na kusema kuwa Democrat ‘walikuwa wanafanya hila” kumshtaki Trump.

“Kesi hii imekuwa maigizo kutoka mwanzo hadi mwisho,” alisema. “Maonesho yote hayajawa chochote isipokuwa harakati isiyo na dhamana na hila za kisiasa za muda mrefu dhidi ya Bw Trump na chama cha upinzani.”

Trump mwenyewe amesema, hakuna rais ”aliyewahi kupitia hatua kama hii na kuwa ” harakati za kuifanya Marekani kuwa kubwa tena” ndio kwanza zimeanza.”

Awali Maseneta walipiga kura kwa ushuhuda binafsi, ambao ungechelewesha uamuzi wa Jumamosi. Lakini baada ya mashauriano ya dharura walibadilisha uamuzi wao kukubali taarifa zilizoandikwa tu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!