July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dola 36 mil kusaidia uvuvi

Spread the love

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imepokea Dola za Marekani milioni 36 kupitia Mradi wa Uvuvi Ukanda wa Bahari ya Hindi (SWIOFISH). Anaandika Faki sosi … (endelea).

Mradi huo utakaotekelezwa ndani miaka sita kwa awamu tatu, umelenga kuimarisha usimamizi madhubuti wa uvuvi katika ngazi ya kanda, kitaifa na kijamii.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Judith Mhina alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa ukuzaji wa viumbe bahari Tanzania Bara.

Mhina amesema kuwa, mradi huo utafanya stadi ya kujua mahitaji halisi ya wadau ambapo mradi huo utapitia muongozo wa uwekezaji katika ukuzaji viumbe kwenye maji bahari, ikiwa na lengo la kuwawezesha wawekezaji kufahamu taratibu za kutafuta uwekezaji kwenye maeneo hayo.

“Maeneo yatakayohusika kwenye mradi huo ni Mafia, Mheza, Kinondoni, Kilwa, Temeke, Mtwara mjini na vijijini, Lindi, Ilala na Rufiji ambayo muwekezaji ataweza kuhusishwa,” amesema Mhina.

Amesema kuwa mradi huo utasaidia kukomesha uvuvi haramu wa kutumia mabomu kwa kushirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii, Nishati na Madini, Mambo ya Ndani na Wizara ya Katiba na Sheria.

Ametaja mashirka yaliyochangia kiasi kitakachoweza kusaidia mradi huo kuwa ni Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF), uliochangia dola 5,000,000, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo (IDA), dola 31,000,000 hivyo jumla ya fedha zote zilizochangiwa ni dola 36,000,000.

Tanzania Bara ilipatiwa dola 17,280,000, Visiwani Zanzibar dola 11,520,000 na Mamlaka ya Usimaizi wa Uvuvi katika Bahari Kuu ilipewa dola 7,2000,000.

error: Content is protected !!