April 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dodoma wasaka mwarobaini ufaulu wa wanafunzi

Dk. Binirith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Spread the love

KASIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatarajiwa kuwa ngeni rasmi katika uzinduzi wa Kongamano la Elimu Mkoa wa Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa Dk. Binirith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kongamano hilo litafanyika tarehe 21 – 22 Machi 2020, katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango jijini humo.

Dk. Mahenge amesema, kongamano hilo litahusisha wadau wa elimu, kwa lengo la kujadili juu ya kushuka kwa elimu katika mkoa wa Dodoma, sambamba na kutafuta njia ya kuiboresha elimu.

Amesema, kongamano hilo litajielekeza zaidi kujua ni kwanini wanafunzi wamekuwa wakifanya vibaya shuleni, pia kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa changamoto kwa wanafunzi wa mkoa huo.

“Msukumo wa kuandaa kongamano hili umetokana na ukweli, kuwa hali ya maendeleoya elimu siyo nzuri na ufaulu kimkoa siyo wa kudhisha. Vipo baadhi ya viashiria ambavyo tumevibaini tukaona vinapelekea kushuka kwa kiwancha elimu mkoani,” amesema Dk. Mahenge.

error: Content is protected !!