January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dodoma wahaha kupata maji

Spread the love

WANANCHI wa mji wa Dodoma wameonja joto ya jiwe kwa kukosa maji kwa siku mbili mfululizo huku wakihofia tatizo hilo linaweza kuwasababishia kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa ni tishio kwa kila kona ya nchi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo ya kukosemana kwa maji katika mji wa Dodoma inatokana na kuwepo kwa tangazo la Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira, kueleza kuwa kutokana na kuwepo kwa tatizo la umeme kunasababisha kutopatikana kwa maji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Mkazi mmoja wa Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Yahana amesema kitendo cha kukosekana kwa maji kwa siku mbili mfululizo kimesababisha hali ya usafi kuwa mbaya ukizingatia kwamba nyumba nyingi zinatua vyoo vya ndani.

“Kwa sasa mji wa Dodoma na maeneo mbalimbali yanakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu hivyo ni hatari kubwa kukosemaka kwa maji safi,” amesema Mariam.

Mariam alieleza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi kwa wale wenye watoto wadogo kwani nguo za kuwabadilisha zimekuwa zikichafuka huku hakuna jinsi yoyote ya kufanya usafi.

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa, Mhandisi Kashilimu Mayunga amesema tatizo hilo linatokana na kuwepo kwa matatizo ya umeme ambao umekuwa ukikatwa na Tanesco.

Alisema hali hiyo katika mji wa Dodoma imesababisha wananchi kukosekana kwa maji na hivyo kuwashauri wale wenye vifaa kuweka maji ya akiba.

error: Content is protected !!