Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Dodoma haina shida ya ujenzi wa majengo marefu
Habari Mchanganyiko

Dodoma haina shida ya ujenzi wa majengo marefu

Spread the love

 

SERIKALI imesema haijawahi kutangaza kuwa mkoa wa Dodoma haufai kujengwa majengo marefu kwa sababu ya kutitia kama ilivyokuwa ikivumishwa na watu ambao hawakuwa na taarifa rasmi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). 

Hayo yamebainishwa leo tarehe 12 Februari 2023 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dk. Matiko Mturi alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.

Akijibu maswali ya wanahabari muda mfupi baada ya kuwasilisha taarifa yake ya utekelezaji alisema kuwa si kweli kuwa Jiji la Dodoma haufai kujengwa majengo makubwa na marefu bali ni suala la upangaji wa makazi ambao unafanywa na jiji husika.

“Kumekuwepo na uvumi kuwa Dodoma haistahili kujengwa majengo marefu kutokana na kuwa na maji mengi chini kutokana na kuwepo kwa kauli hiyo wewe ukiwa mshauri na mtendaji wa baraza la taifa la ujenzi unatoa kauli gani ili tuweze kuwa na uhakika wa hizi kauli au kuwahabarisha wananchi ambao wengine wanaweza kuwa na hofu,” aliuliza mmoja wa wanahabari.

Akijibu swali hilo Dk. Mturi amesema kuwa siyo kweli kuwa Dodoma haistahili kujenga majengo marefu, ila kila sehemu uweza kujengwa kulingana na teknolojia ya eneo husika.

“Nataka kujua nani aliyewahi kusema kuwa Dodoma haiwezi kujengwa majengo marefu wala makubwa isipokuwa kama kuna sehemu yenye matetemeko basi ujenzi ufuata teknologia iliyopo na iwapo majengo ujengwa kwa ukanda utegemea mpangilio wa halmahauri au majiji kwa nia ya mpangilio wa kupendezesha mji kwa maana ya kuamua kuwa ni wapi yajengwe magorofa, nyumba fupi au nyumba za aina fulani,” amefafanua Dk. Mturi.

Akizungumzia majukumu ya baraza amesema kuwa baraza linatekeleza majukumu tisa ambayo ameyataja kuwa ni kukamilisha mwongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchi nzima kwa kuandaa gharama za msingi za makandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa Tanzania Bara.

Ametaja majukumu mengine kuwa ni kuandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na miongozo inayosimamia ujenzi wa majengo nchini.

Aidha amesema kuwa viwango mswazo ya majengo ya serikali, kutoa mafunzo kujenga uwezo wa wadau wa sekta ya ujenzi nchini, kutoa fahirisi za bei za vifaa, mitambo na ujura katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kuonesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi na mambo mengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!