Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk Tulia: Rais Samia amefanya na zaidi
Habari za Siasa

Dk Tulia: Rais Samia amefanya na zaidi

Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kasi ya utekelezaji wa miradi inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inamfanya amuone anafanya zaidi. Anaripoti Seleman Msuya, Rufiji, Pwani … (endelea). 

Dk Tulia amesema hayo leo Alhamisi tarehe 22 Desemba, 2022, wakati akizungumza mbele ya Rais Samia kwenye hafla ya zoezi la ujazaji maji katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), iliyofanyika Rufiji mkoani Pwani.

Spika Tulia amesema baada ya kupita na kuangalia shughuli zilizofanyika ametambua kuwa kazi kubwa imefanyika kwa kipindi kifupi cha Rais Samia.

“Mimi nadiriki kusema Rais Samia umefanya, unafanya na kuzidi kwani mradi huu umefikia sehemu nzuri ya kupongezwa,”amesema.

Amesema mradi huo kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 70 hivyo ni matumaini yake utaisha katika muda uliopangwa.

Dk Tulia amesema yeye kama kiongozi wa Muhimili wa Bunge atahakikisha unazungumziwa vizuri ndani na nje ya Bunge.

“Bunge litaendelea kuunga mkono miradi yote ambayo inatekelezwa nchini, ukiwemo huu wa JNHPP ambao unaenda kukuza uchumi wetu siku zijazo,”amesema.

Spika Tulia amesema ni imani yake mradi huo utaenda kugusa sekta zingine na nchini kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!