October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Tulia: Nendeni mahakamani

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia amewataka wabunge wanaodai kuchafuliwa kwa kuandikwa hovyo na baadhi ya magazeti, waende kushitaki mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema kuwa, Bunge halistahili kuingilia mambo hayo kama ambavyo imeombwa na Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda (Chadema).

Mbunge huyo leo tarehe 24 Juni 2019, ameomba kiti cha spika kuingilia kati sakata la wabunge kuchafuliwa akisema kwamba, kadhia hiyo inachafua muhimili huo.

Mwambi amelieleza Bunge kuwa, magazeti hayo yamekuwa yakituhumu wabunge kuhusika na vitendo vya rushwa na baadaye kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

“Suku hizi kuna vigazeti vimekuwa vikiwachafua wabunge, hasa pale linapotokea jambo la kitaifa,” amesema Mwambi na kuongeza: Lipo lililotaja wabunge kuhusika na rushwa, kwanini wahariri wake wasiitwe kujieleza katika kamati ya maadili?”

Hata hivyo, Dk. Tulia amesema kuwa, suala hilo halijatokea bungeni hivyo haliwajibiki na badala yake, wahusika wakiona kama kuna umuhimu basi wawapeleke mahakamani.

Hivi karibuni Mwambi na Hussein Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega Mjini, walishambulia magazeti hayo likiwemo Tanzanite kwa madai ya kuandika habari walizoita za hovyo na zisizofuata maadili.

error: Content is protected !!