SPIKA wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa asilimia 60.5 ya fedha zilizotengwa katika bajeti ya 2021/2022, katika kipindi cha muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Spika Tulia amesema hayo leo Jumamosi, tarehe 19 Machi 2022, akifungua kongamano la tathmini ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, lililofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma.
“Kwa ujumla ukifanya tathimini ya hizi takwimu unapata wastani wa asilimia 60.5 kutoka Julai 2021 mpaka kufikia Januari 2022. Hizi ni asilimia kubwa sana ukilinganisha na vipindi vingine,” amesema Spika Tulia.
Spika Tulia amesema, Wizara ya Afya imepokea asilimia 62.32, wakati Wizara ya Maji ikipokea asilimia 76.51 huku Wizara ya Maliasili na Utalii ikipokea asilimia 58.08. Wizara ya Ujenzi (60.69), Uchukuzi (23.32), Wizara ya Elimu (69.31) na Ofisi ya Rais-TAMISEMI (36.46).
Leave a comment