SPIKA wa Bunge, Dk.Tulia Ackson ameamuru kuondolewa kwenye kumbukumbu za bunge Hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 baada ya kuvutana na waziri kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Sugu kulalamika na kugoma kusoma hotuba aliyowekewa mezani kwa madai kuwa, hotuba hiyo siyo ile iliyoandaliwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Hotuba hiyo ambayo ilitakiwa kuwasilishwa na Sugu, aliigomea licha ya Dk.Tulia kutaka aendelee kusoma hiyo hiyo.
Katika msuguano huo Sugu amesema, hawezi kusoma hotuba hiyo kwa kuwa, alichopaswa kusoma ndani ya ukumbi wa bunge si maoni yake bali ya upinzani. Amesisitiza kuwa “siwezi kulishwa maneno.”
Sugu amelalamika kuwa, imekuwa kawaida ya kiti cha spika kutaka kuizuia hotuba ya yake ili asiweze kuisoma akidai ni dalili za uoga wa serikali.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Akson alisema kitendo cha Sugu kutowasilisha hotuba yake bungeni, hakitakuwa katika kumbukumbu za taarifa za Bunge.
Leave a comment