September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Tulia ajiuzulu U-naibu Spika

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

 

DAKTARI Tulia Ackson, ametangaza kujiuzulu nafasi ya naibu spika wa Bunge la Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa ya kujiuzulu kwake imetangazwa leo Jumanne, tarehe 1 Februari 2022, Bungeni jijini Dodoma na Katibu wa Bunge la Tanzania, Nenelwa Mwihambi.

Nenelwa amesema, jana Jumatatu 31 Januari 2022 saa 12:00 jioni, alipokea barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akidai amepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya spika.

Awali, katibu huyo wa Bunge, alisoma taarifa ya Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi ya spika akisema, alipokea barua ya Ndugai tarehe 6 Januari 2022 hivyo nafasi hiyo ilikuwa wazi kuanzia siku hiyo.

Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya kauli yake ya kukosoa kuhusu serikali kuendelea kukopa fedha kugharamikia miradi ya maendeleo kuibua mjadala mkali ndani ya CCM na kushinikizwa kujiuzulu naye akafanya hivyo.

error: Content is protected !!