September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Tizeba: Watanzania wale nyama

Spread the love

SERIKALI inafikiria jinsi ya kuanzisha kampeini ya uhamasishaji ya Watanzania kula nyama ya ng’ombe, mbuzi na mifugo mingine inayoliwa, anaandika Dany Tibason.

Imeelezwa kuwa, licha ya Tanzania kuwa ya tatu katika kuwa na mifugo mingi barani Afrika, lakini  ni ya tatu kutoka mwisho katika ulaji wa nyama.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Dk.Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi alipokuwa akifungua maonesho ya mifugo kitaifa yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nane Nane, Nzuguni mkoani Dodoma.

Dk. Tizeba amesema, kutokana na hali hiyo serikali inafikiria kuanzisha kampeini ya utoaji na uhamasishaji kwa Watanzania kula nyama kwa wingi.

Mbali na hilo amewataka wafugaji kufunga kwa malengo ya kibiashara badala ya kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija.

“Ifike sasa hatua ya wafugaji kufanya ufugaji wenye tija badala ya kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija yoyote.

“Haina maana kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija yoyote nabado mfugaji huyo anaendelea kuwa masikini, mfugaji huyo hana nyumba mzuri” ameeleza Dk. Tizeba.

error: Content is protected !!